Skip to main content

Baraza la usalama lajadili operesheni za UM nchini Somalia

Baraza la usalama lajadili operesheni za UM nchini Somalia

Baraza la usalama leo limekutana kufanya mashauriano kuhusu Somalia, ambapo wajumbe wa baraza hilo wamsikiliza taarifa ya makakati wa usaidizi wa operesheni za  ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia UNSOA katika vikosi vya nchi hiyo. Taarifa zaidi na Abdullahi Boru.

(TAARIFA ABDULLAHI)

Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu operesheni za ulinziu wa amani Atul Khare ameliambia baraza hilo kuwa UNSOA imefanya kazi katika mazingira magumu kwa kukabiliana na upinzani mkali kutoka kwa kundi la kigaidi la Al Shabaab akitolea mfano kuwa katika kipindi cha majuma 13 yaliyopita UNSOA imeshambuliwa kwa wastani wa mara moja kwa kila majuma kumi.

Amesema mashambulizi hayo yanalenga mali za UNSOA au wafanyakazi wake na hivyo kuhatarisha usalama wao. Hata hivyo amesema kwa kushirikiana na ujumbe wa muungano wa Afrika nchini Somalia AMISOM, UNSOA imeendelea na operesheni za ulinzi wa amani lakini kuna mengi ya kufanya.

(SAUTI ATUL KHARE)

‘Ili kusonga mbele UNSOA inahitaji kuimarishwa . Wakati sekretarieti itakuwa inatimiza majuku yake, msaada muhimu utahitajika kutoka baraza la usalama  , baraza kuu na bila shaka yoyote Muungano wa Afrika.’’

Awali baraza la usalama lili[pitisha azimio la kuongeza muda wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti MINUSTAH kwa mwaka mmoja.