Skip to main content

Biashara ndogo na za wastani ni kiungo muhimu katika ukuaji endelevu wa uchumi- ITC

Biashara ndogo na za wastani ni kiungo muhimu katika ukuaji endelevu wa uchumi- ITC

Biashara za kimo kidogo na cha kati, SMEs ni kiungo muhimu kinachokosa kwa ajili ya ukuaji endelevu wa uchumi, kwani biashara hizo ni kichochezi muhimu katika kuhakikisha ushirikishwaji mkubwa. Hii ni kwa mujibu wa ripoti mpya kuhusu SME ya 2015, iliyotolewa leo mjini Geneva na Shirika la Kimataifa la Biashara, ITC. Assumpta Massoi anatuarifu zaidi.

(Taarifa Assumpta)

Mada kuu na muhimu ya ripoti hiyo ni uunganishwaji, ushindani na mabadiliko kwa ukuaji jumuishi.

Katika mazingira yasiyotabirika ya ukuaji wa uchumi wa dunia, ripoti hiyo inaonyesha kwamba kuongeza tija ya SME itapelekea uzalishaji zaidi na ajira kubwa, itakayosambazawa katika maeneo yasiyo na ukuaji mkubwa wa kiuchumi.

Aidha, ripoti hiyo inaelezea pia kupanuliwa kwa SME’s kimataifa kutachangia biashara na uwekezaji ambao utaongeza tija ya juu, mapato makubwa, na fursa nyingi za ajira.