Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjadala wa mabadiliko ya tabianchi ujumuishe kilimo: FAO

Mjadala wa mabadiliko ya tabianchi ujumuishe kilimo: FAO

Nchi zote zinapaswa kuhakikisha kuwa suala la uhakika wa chakula na kilimo yanapatiwa kipaumbele katika mjadala wa mkataba mpya wa mabadiliko ya tabianchi utakaopitishwa mwishoni mwa mwaka huu huko Paris, Ufaransa.

Hiyo ni kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa shirika la chakula na kilimo duniani, FAP José Graziano da Silva na Waziri wa kilimo wa Ufaransa Stéphane Le Foll walipokuwa wakizungumza huko Roma Italia kando mwa maadhimisho ya wiki ya chakula duniani.

Bwana da Silva pamoja kupitia chepuo ajenda ya maendeleo endelevu, amesema mafanikio yake yanataka kubadilishwa kwa mifumo ya kilimo na ile ya uzalishaji chakula ili iweze kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Amesema dunia inafahamu inaweza kutokomeza njaa ifikapo mwaka 2030, lakini inafahamu pia mabadiliko ya tabianchi yanatishia jitihada hizo na hivyo sekta za kilimo, uvuvi ni lazima zizingatiwa katika kustahimili mabadiliko hayo.

Kwa upande wake Waziri Le Foll amesema mara nyingi kilimo kinalaumiwa kwa kutoa gesi chafuzi lakini ni lazima mbinu mpya zibuniwe ili kilimo kiweze kuwa rafiki kwa mazingira na hivyo kusaidia kufanikisha malengo endelevu.