Kemeeni machafuko kulinda urithi wa tamaduni: UNESCO

27 Septemba 2015

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa elimu, sayansi na utamaduni UNESCO Irina Bokova ametaka nchi wanachama wa UM kusimama kinyume na wale wenye nia ya kuleta migawanyiko, utengano na machafuko akisema mambo hayo huchangia kurudisha nyuma harakati za kuhifadhi urithi wa kitamaduni.

Akizungumza katika mjadala kuhusu ulinzi wa kitamaduni kwa mnaufaa ya historia ya binadamu  mjini New York, Bi Bokova amewaambia wadau mbalimbali wakiwemo wawakilishi wa nchi na mashirika ya kimataifa kuwa nchi zina mamlaka na uwezo wa kulinda urithi wa kitamaduni na akatoa hakikisho.

(SAUTI BOKOVA)

"UNESCO ipo imara ili kukomesha misimamo mikali, ugaidi, kwasababu naamini haya ni miongoni mwa matishio makubwa ynayomkabili mwanadamu na Umoja wa Mataifa leo.’’

Amesema wakati wa kutekeleza ulinzi wa urithi wa kitamaduni muhimu tofauti katika misingi ya imani na dini zikaheshimiwa kwa kuzingatia haki za binadamu.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter