Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sekta ya benki yaombwa kuchangia zaidi katika mabadiliko ya uchumi rafiki kwa mazingira

Sekta ya benki yaombwa kuchangia zaidi katika mabadiliko ya uchumi rafiki kwa mazingira

Wakati ambapo watalaam wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi wanakutana wiki hii mjini New York, Marekani, Kamishna Mkuu wa France Strategie, idara ya mikakati na yanayotazamiwa ya Ufaransa, Jean Pisani, amesema ufadhili katika kubadilisha uchumi ili utumie gesi yenye uchafuzi mdogo unapaswa kuwa mkubwa na kuwa na mtazamo wa mbali.

Amesema hayo akiongoza mjadala maalum kuhusu mchango wa sekta ya benki katika kubadilisha uchumi kuelekea uchumi unaotumia gesi yenye uchafuzi mdogo.

Lengo la mkutano huo ni kubuni mikakati au ufadhili ili kuwekeza katika miradi inayotumia kaboni kidogo, wakati ambapo sekta binafsi, serikali na sekta ya benki zinakumbwa na changamoto za kiuchumi.

"Kwenye hali ya sasa ambapo uchumi unaimarika pole na watu hawajaridhika na ukuaji wa uchumi duniani, michango mikubwa zaidi katika kubadilisha uchumi ingeweza kuwa suluhu kwa hali ya uchumi inayozungumziwa sasa."