Skip to main content

Hungary inavunja sheria ya kimataifa kwa kufurusha wakimbizi: Zeid

Hungary inavunja sheria ya kimataifa kwa kufurusha wakimbizi: Zeid

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu Zeid Ra’ad Al Hussein amesema amesikitishwa sana na vitendo vilivyofanywa na serikali ya Hungary na mamlaka zake za kuwakataza wakimbizi kuingia nchini humo, kuwafunga na kutumia nguvu dhidi yao, akisema baadhi ya vitendo vyao vinaweza kuwa ni ukiukaji wa sheria ya kimataifa.

Kamishna Zeid amesema hayo kwenye taarifa iliyotolewa leo wakati ambapo serikali ya Hungary inajenga ukuta mpakani, wa kudhibiti uhamiaji kutoka Serbia, na ikiwa imepitisha sheria mpya ya kuadhibu uhamiaji haramu nchini humo.

Huku Waziri Mkuu wa Hungary Victor Orban akisema harakati hizo zinalenga kutunza mila zao ambazo haziingiliani na dini ya kiislamu, Kamishna Zeid amelaani mtazamo huo wa kibaguzi.