Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF na WFP waongeza jitihada za kumaliza utapiamlo Sudan Kusini

UNICEF na WFP waongeza jitihada za kumaliza utapiamlo Sudan Kusini

Shirika la Mpango wa Chakula, WFP na Shirika la Kuhudumia Watoto, UNICEF, leo yamezindua mpango uloimarishwa wa kupambana na hali mbaya ya utapiamlo nchini Sudan Kusini, ambako mgogoro umelazimu mamilioni ya watu kuhama makwao, huku ukiharibu huduma za msingi na kuongeza magonjwa na njaa. Taarifa kamili na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Mpango huo wa pamoja wa lishe utawezesha mashirika hayo na wadau kuwasaidia zaidi ya watu milioni mbili katika kutibu na kuzuia utapiamlo hadi mwezi Mei mwaka 2016, ukilenga hasa watoto, waja wazito na waliojifungua karibuni.

Mashirika hayo mawili yalianzisha mkakati wa pamoja wa lishe mwaka jana, na sasa yanaanza mwaka wake wa pili, yakilenga kupanua kazi yao ya kuokoa maisha.

Kwa mujibu wa UNICEF, mtoto mmoja hupata utapiamlo uliokithiri nchini Sudan Kusini kila dakika mbili zipitazo, huku ripoti ikionyesha kuwa hatua zilizochukuliwa mwaka jana ziliyawezesha mashirika hayo kuwafikia watu milioni moja kote nchini na kuepusha njaa.