Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwezo wa kusoma na kuandika ni ufunguo kwa maendeleo endelevu: UNESCO

Uwezo wa kusoma na kuandika ni ufunguo kwa maendeleo endelevu: UNESCO

Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kutokomeza ujinga wa kutokujua kusoma na kuandika, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO Irina Bokova amesema uwezo wa kusoma na kuandika ni ufunguo kwa maendeleo endelevu na jamii jumuishi.  Grace Kaneiya anafafanua zaidi.

(Taarifa ya Grace)

Kwenye ujumbe wake kwa siku hiyo Bi Bokova amesema licha ya mafanikio makubwa yaliyopatikana tangu mwaka 2000 katika kupunguza ujinga wa kutokujua kusoma na kuandika bado watu zaidi ya milioni 750 duniani kote hawajui kusoma wala kuandika, theluthi mbili wakiwa ni wanawake.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema uwezo wa kusoma na kuandika ni muhimu sana katika kuhamasisha binadamu na kutekeleza ajenda ya maendeleo ya mwaka 2030.

Maadhimisho ya siku hiyo ya kimataifa yatafanyika leo na kesho mjini Paris Ufaransa kwenye makao makuu ya UNESCO.