Skip to main content

UNRWA yashukuru nchi zilizosaidia upungufu wa fedha

UNRWA yashukuru nchi zilizosaidia upungufu wa fedha

Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA Pierre Krähenbühl ameelzea shukrani zake za dhati kutokana na usaidizi wa mfano, na uelewa kutoka nchi wenyeji,  wakati shirika hilo likihaha kufunga nakisi ya bajeti yake kufuatia upungufu katika miezi ya hivi karibuni.

Katika taarifa yake, Bwana Krähenbühl  amezishukuru serikalia za Jordan kwa usaidizi mkuu, pamoja na Palestina hususani shirika la la ukombozi kupitia kitengo cha masuala ya wakimbizi, huku pia akielekeza shukrani kwa Lebanon kwa usaidizi.

UNRWA imeshukuru majadiliano iliyoyafanya na Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya wakimbizi wa Palestina  wenye asili ya Kiarabu kuhusu mkwamo wa kifedha ambao ulilikumba shirika hilo.

Kamishna huyo wa UNRWA amekariri wito wake kuwa elimu ni haki ya msingi kwa watoto popote  pale na kuongeza kuwa lazima kuhakikisha hali hiyo ya ukosefu wa fedha kwa huduma muhimu kama hiyo haijirudii tena.