Skip to main content

Raia wasibughudhiwe wakidai haki kwa amani: UM

Raia wasibughudhiwe wakidai haki kwa amani: UM

Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Lebanon Bi Sigrid Kaag, amezingatia maandamano ya hivi karibuni ya raia nchini humo ya kudai huduma msingi na utendaji kazi makini wa serikali.

Katika taarifa yake Bi Kaag amesisitiza umuhimu wa ulinzi wa haki za raia wakati wa kuelezea matarajio na madai yao kwa njia ya amani na kulezea kusikitishwa kwake kufuatia machafuko na uharibifu wa mali za uma katika maandamano ya hapo jana.

Martibu huyo ameelezea masikitiko yake kuhusu kifo cha muandamanaji mmoja na majeruhi kadhaa na akataka pande zote kujizuia.

Kadhalika ameelezea kuridhishwa kwake na juhudi za Waziri Mkuu wa Lebanon Tamam Salam za kupigia chapuo makubaliano ya kisiasa na akakariri wito wake uwajibikaji wa viongozi kwa raia.