Baraza la usalama lalaani utekaji wa Ubalozi wa UAE Sana'a, Yemen

Baraza la usalama lalaani utekaji wa Ubalozi wa UAE Sana'a, Yemen

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wamelaani vikali uvamizi na utekaji wa ubalozi wa Falme za Kiarabu, UAE mjini Sana’a, Yemen, uliofanywa na wapiganaji wa Houthi mnamo Ahosti 17, 2015.

Wajumbe hao wamewataka wapiganaji wote wa Houthi waondoke mara moja kwenye majengo ya ubalozi huo.

Aidha, wamelaani vitendo vyote vya ghasia dhidi ya majengo ya kidiplomasia, wakikumbusha kanuni ya kutovamia majengo ya kibalozi. Wamekumbusha pia kuhusu wajibu wa serikali wenyeji kuchukua hatua zote zinazohitajika kulinda majengo ya kidiplomasia dhidi ya uvamizi au uharibifu, au hata mashambulizi dhidi ya mawakala wa kidiplomasia na maafisa wa ubalozi.