Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNRWA yatangaza mwaka wa masomo 2015-2016

UNRWA yatangaza mwaka wa masomo 2015-2016

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA), limetangaza ufunguzi wa shule zake Palestina, Jordan, Lebanon na Syria, baada ya kuchelewa kwa muda juu ya pengo la ufadhili. Taarifa kamili na John Kibego.

(Taarifa ya Kibego)

Katika kauli yake Kamishina Mkuu wa UNRWA Pierre Krähenbühl (Piekh Kraenbul) amesema, wanafunzi nchini Palestina watarudi shueleni tarehe 24 mwezi huu wa Agosti kuanza mwaka wa elimu wa 2015/16, huku Jordan wakifungua tarehe mosi Septemba.

Nchini Syria shule zitafunguliwa tarehe 13 Septemba, baada ya Lebanon kufungua tarehe 7 Septemba.

Kamishna Krähenbühl amesema amechukua uamuzi huu kutokana umuhimu wa elimu kwa wakimbizi wa Kipalestinana wavulana na wasichana 500,000, ambao mustakbali wao unategemea elimu na ujenzi wa ujuzi katika shule 685 zinazosaidiwa na UNRWA.

Kamishina huyo amesisitiza kuwa dunia haiwezi kukubali hatari ya wanafunzi hao kuendelea bila elimu.