Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana watakiwa kuamka kuchangamkia fursa

Vijana watakiwa kuamka kuchangamkia fursa

Kuelekea siku ya kimataifa ya vijana hapo kesho Agosti 12, vijana wametakiwa kuacha kulalamika badala yake kutumia fursa zilizopo kujikwamua kiuchumi na kijamii.

Katika mahojano na idhaa hii kijana Anganile Mwakyanjala aliyekuja hapa Marekani kuhudhuria mkutano kuhusu vijana wa Afrika uliomalizika mjini Washington, anasema  vijana wanaweza ikiwa.

(SAUTI ANGANILE)

Siku ya vijana duniani iliyopitishwa na baraza kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 1999 inalenga zaidi katika wajibu wa vijana wa kiume na wanawake katika kuleta mabadiliko na elimu kuhusu changamoto zinazowakabili.