Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN Habitat yazindua mtandao wa ubia na vyuo vikuu

UN Habitat yazindua mtandao wa ubia na vyuo vikuu

Tovuti mpya imezinduliwa na Shirika la Makazi katika Umoja wa Mataifa, UN Habitat ili kutoa jukwaa la kuendeleza ubia wa karibu baina ya vyuo vikuu na miji.

Inatarajiwa kuwa ubia huo utaongeza ushiriki wa vyuo vikuu katika kutatua matatizo ya makazi, na hivyo kuchagiza mafunzo ya ushirikiano.

Jukwaa hilo ambalo ni sehemu ya Mtandao wa mkakati wa vyuo vikuu wa UN Habitat, UNI, unaalika vyuo vikuu, wahadhiri na wanafunzi kuungana na wadau wa vyuo zaidi ya 180 duniani katika ushirikiano wao wa kujenga miji endelevu.

Jukwaa hilo jipya litawawezesha watumiaji kusoma tathmini, habari na fursa za ushirikiano wa wadau wa UNI, na kubadilishana mawazo kuhusu masuala kama vile ya jinsia na miji salama zaidi, na pia kufuatilia maandalizi ya mkutano wa Habitat III na ajenda mpya ya miji.