Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya watu wa asili kuadhimishwa leo

Siku ya watu wa asili kuadhimishwa leo

Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya watu wa asili yatafanyika baadaye hii leo hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa yakilenga afya na ustawi wa kundi hilo. Joshua Mmali na maelezo kamili.

(TAARIFA YA JOSHUA)

Siku hiyo huadhimishwa kila Agosti tisa na kutoa fursa kwa wadau wa haki za binadamu wakiwamo watu wa asili wenyewe kujadili mustakabali wao ambapo Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon katika ujumbe wake wa kuadhimisha siku ya watu wa asili amesema jamii hiyo haitaachwa nyuma katika ajenda ya  maendeleo baada ya mwaka 2015.

Katika mahojiano na idhaa hii Dk Priscilla Migiro ambaye ni daktari wa watoto mwenye asili ya Wamasai kutoka Kenya anasema

(SAUTI YA MIGIRO)

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa bado watu wa asili wanakumbwa na changamoto kadhaa kwa upande wa afya, ikiwa ni ukosefu wa huduma za afya ya uzazi, ukatili wa kijinsia, kiwango cha juu cha visa vya ugonjwa wa sukari na matumizi ya madawa ya kulevya na pombe, akieleza kwamba matatizo hayo mengi yanazuilika.