Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afya na ustawi wa watu wa asili wamulikwa

Afya na ustawi wa watu wa asili wamulikwa

Mfuko wa kujitolea wa Umoja wa Mataifa kuhusu watu wa asili kwa kushirikaiana na kundi la wataalamu wametoa ujumbe kuhusu haki za kundi hilo kuelekea maadhimisho ya kimataifa ya siku ya  jamii za watu wa asili mnamo Agosti tisa.

Katika ujumbe huo wa pamoja vyombo hivyo vinasema siku hiyo inatoa fursa kwa jumuiya ya kimataifa kuendelea kuzingatia haki za binadamu za jamii hizo na maendelao katika kutimiza tamko la UM kuhusu haki za  watu wa asili.

Ujumbe wa mwaka huu ni kuelekea malengo endelevu baada ya 2015 kuhakikisha afya za watu asili katika afya na ustawi wao. Elifuraha Lataika  ni mwakilishi wa jamii ya watu wa asili kutoka Tanzania na mhadhiri katika chuo kikuu cha Tumaini Makumira anazungumzia umuhimu wa maadhimisho hayo.

(SAUTI ELIFURAHA)