Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usafirishaji haramu wa binadamu wapingwa Tanzania

Usafirishaji haramu wa binadamu wapingwa Tanzania

Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania imeungana na nchi na taasisi nyingine duniani,  kuadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga usafirishji wa kibinadamu,  kwa kuwajumuisha wadau mbalimbali ili kujadili mbinu za kukomesha biashara hiyo.

Maadhiimisho hayo yaliyowaleta pamoja shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, watunga sera na vyombo vya utekelezaji wa sheria yalishuhudia mjadala na elimu juuya ukubwa wa tatizo hilo. Ungana na Priscilla Lecomte katika makala ifuatayo.