Sauti kutoka kona mbali zadhihirisha umuhimu wa chombo:Radio
Mwaka huu 2014, siku ya Radio duniani imeangazia uwezeshaji wa kijinsia kupitia Radio, iwe kwa kuajiri wanawake kama viongozi kwenye sekta hiyo au watendaji au kuandaa vipindi ambavyo vinajenga usawa wa kijinsia kwa kuboresha maisha ya wanawake na watoto wa kike kiuchumi, kisiasa na kijamii. Ni katika muktadha huo ambapo Idhaa hii imekusanya taarifa kutoka kona mbali mbali zinazoonyesha namna wanawake hususan barani Afrika wanavyonufaika na uwepo wa radio pale walipo.