Siku ya kimataifa ya Mandela yaadhimishwa katika Umoja wa Mataifa

Siku ya kimataifa ya Mandela yaadhimishwa katika Umoja wa Mataifa

Hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Nelson Mandela ambayo iliadhimishwa rasmi mnamo tarehe 18 mwezi Julai siku aliyozaliwa.Taarifa kamili na Joseph Msami

(TAARIFA YA MSAMI)

Kwa mara ya kwanza siku hii imeadhimishwa katika Umoja wa Mataifa kumeunzi marehemu Mandela Rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini na mpigania uhuru na aliyepambana na ubaguzi wa rangi ambaye aliyefariki dunia Desemba tano mwaka 2013.

Akiongea katika tukio hilo Rais wa baraza kuu Sam Kutesa ameelezea umuhimu wa Nelson Mandela jabali la Afrika na dunia.

(SAUTI KUTESA)

Maadhimisho haya yamekwenda sambamba na utolewaji tuzo za kwanza ziitwazo Nelson Rolihlahla Mandela zitakazotolewa na Umoja wa Mataifa kila mwaka ambapo waliopokea tuzo hizo hii leo ni Dk Hellena Ndome daktrai wa mcgho kutoka Namibia na Rais msataafu wa Ureno Jorde Sampio.

Katika mahojiano maalum na redio ya Umoja wa Mataifa kabla ya kupokea tuzo Dk Ndume ameelezea mkasa wa mama aliyepata upofu na kutibiwa kisha kupona akisema.

(SAUTI DK NDUME)

"Ajuza huyu mwanamke alikuwa na watoto watatu, na wote walikufa kwa HIV, alisalia na wajukuu na alikuwa haoni. Furaha aliyokuwa nayo baada ya kuona tena ilikuwa ya ajabu. Aliweza kwenda kuwaangalia wajukuu wake. ''