Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Udungaji sindano usio salama wamulikwa katika vita dhidi ya Hepatitis

Udungaji sindano usio salama wamulikwa katika vita dhidi ya Hepatitis

Hatari ya vifo kutokana na homa ya ini au hepatitis, imepunguzwa kwa kiwango kikubwa katika baadhi ya maeneo duniani, lakini bado ni tishio kubwa katika maeneo mengine, limesema Shirika la Afya Duniani, WHO.

Kwa mujibu wa WHO, homa ya ini aina B na C husababisha asilimia 80 ya saratani ya ini, na huua takriban watu milioni 1.4 kila mwaka.

Sababu moja kubwa ya maambukizi ya hepatitis ni udungaji sindano usio salama, katika nchi maskini na nchi tajiri, kama alivyosema Dkt Edward Kelley, katika mahojiano na Redio ya Umoja wa Mataifa.

(Sauti ya Edward Kelley)

"Ni muhimu kushirikisha umma  na jamii. Jamii zinapaswa kuamini kuwa huduma  ya afya wanayopata ni salama na waje katika vituo vya afya, badala ya kwenda kwa vituo binafsi ambako kuna uwezekano wa kupata sindano zisizo salama. Huwezi kudhani tu kwamba kuwaambia watoa huduma wasitoe udungaji usio salama utakuwa na matokeo yoyote, kwani wengi wanafanya hivyo kwa sababu hawapati malipo kwa muda mrefu, na hivyo wanachukua hatua hii ili kukudhi mahitaji ya familia zao."