Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bei ya bidhaa, ukosefu wa nafaka waikumba Yemen: OCHA

Bei ya bidhaa, ukosefu wa nafaka waikumba Yemen: OCHA

Ukosefu wa nafaka kama ngano na gesi ya kupikia, kupanda kwa garama za bidhaa  ni miongopnbimwa madhila yanayowakumba wananchi wa Yemen wakati huu ambapo taifa hili liko katika machafuko.

Kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa Mataif ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA unga wa ngano ambao ndiyo chakula kikuu nchini humo sasa unapatikana kwa bei mara mbili kuliko kawadia huku gesi ya kupikia ikipanda kwa asilimia 264 kwa baadhi ya majimbo.

OCHA imesema kuwa licha ya changamoto kubwa mashirika ya misaada yanasaidia jamii ambazo zina usalama ikitolea mfano wa familia takribani 3,300 zilizopoteza makazi jimboni Sa’ada ambazo tangu kuanza kwa mzozo huo,  zimefikiwa na kupatiwa misaada mathalani mashuka na mahema kwa ajili ya malazi.