Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lakutana kuhusu hali Iraq

Baraza la Usalama lakutana kuhusu hali Iraq

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limekutana kujadili kuhusu hali nchini Iraq, ambapo pia limesikiliza ripoti ya Katibu Mkuu. Taarifa kamili na Joshua Mmali.

(Taarifa ya Joshua)

Ripoti ya Katibu Mkuu imewasilishwa kwenye Baraza la Usalama na Mwakilishi wake maalum Jan Kubis, ambaye pia ni Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq, UNAMI.

Akilihutubia Baraza hilo, Bwana Kubis amesema ingawa harakati za kisiasa zinaendelea nchini Iraq, hazina msukumo unaotakiwa. Amesema gharama ya kibinadamu ya mzozo wa Iraq bado ipo juu sana

Tangu mara ya mwisho nilipolihutibia baraza hili, UNAMI imerekodi vifo vya raia wapatao 1,200 na kujeruhiwa kwa zaidi ya raia 2,000 kutokana na mapigano ya silaha au mashambulizi ya kigaidi. UNAMI inaendelea kupokea ripoti nyingi za mashambulizi dhidi ya raia, mauaji kiholela, utekaji nyara, ubakaji na aina nyingine za ukatili wa kingono, kuwasajili watoto jeshini kwa lazima, uharibifu na uporaji wa mali ya raia, na kutoruhusu raia kufurahia haki za msingi.”

Amesema makundi ya walio wachache, wanawake na watoto wanaendelea kukumbwa na maafa na udhalilishaji unaotekelezwa na kundi linalodai kuweka dola la uislamu wenye msimamo mkali, ISIL.