Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMA yalaani mauaji ya raia Afghanistan

UNAMA yalaani mauaji ya raia Afghanistan

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA umelaani shambulio la bomu lilliosababisha vifo vya watu 19  mapema leo nchini humo. Taarifa zaidi na John kibego.

(Taarifa ya John)

Shambulio hilo lilitokea baada ya bomu kulipuka sokoni kwenye jimbo la Faryab, kaskazini mwa nchi, limejeruhi takribani watu 28.

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Nicholas Haysom amesema shambulio hilo linaonyesha kuwa watekelezaji wa uhalifu huo wanadharau kabisa uhai wa binadamu, akikariri wito wa UNAMA wa kuzuia matumizi ya silaha yanayotumika kwenye maeneo ya makazi.

UNAMA imetuma salamu zake za rambirambi kwa familia za wahanga na kuwatakia nafuu waliojeruhiwa.