Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mji mkongwe Zanzibar waondolewa kwenye orodha ya kutoweka: UNESCO

Mji mkongwe Zanzibar waondolewa kwenye orodha ya kutoweka: UNESCO

Mkutano wa kamati ya urithi wa dunia ya shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO umeridhia kuondoa katika orodha ya kutoweka katika urithi wa dunia mji Mkongwe ulioko Zanzibar  na hatua za kuunusuru mji huo zinaendelea.

Katika mahojiano na idhaa hii Katibu mtendaji wa tume ya taifa ya shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNECSO nchini Tanzania Dkt. Moshi Kiminzi ambaye ni miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo mjini Bone Ujerumani hivi karibuni anaeleza kilichojiri .

(SAUTI KIMINZI)

Kwa mujibu wa Dk Kiminzi UNESCO kwa kuhirikiana na serikali ya Zanzibar wako katika juhudi za kunusuru mji huo kwa kurejesha hadhi ya muonekano wake wa awali na hatua ambazo pia zinaungwa mkono na ngazi ya kimataifa ya shirika hilo.