Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usalama DRC unahitaji ushirikiano kati ya MONUSCO na FARDC : Kobler

Usalama DRC unahitaji ushirikiano kati ya MONUSCO na FARDC : Kobler

Hali  ya usalama nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo DRC inahitaji ushirikiano  kati ya kikosi cha  ulinzi wa amani MONUSCO na jeshi la nchi dhidi ya vikosi vya FDLR amesema Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC Martin Kobler. Tarifa zaidi na Grace Kaneiya

(TAARIFA YA GRACE)

Akihutubia baraza la usalama Kobler amesema kumekuwa na matukio kadhaa yanayotishia usalama wa wananchi wa DRC  kama vile ubakaji na mauaji ambayo yanaelekea kuwa kawaida huku akisema tangu mwaka 2014 mamia ya raia wamefariki dunia kutokana na machafuko .

Kuhusu uchaguzi wa Rais na wabunge mwaka 2016 nchni humo amesema licha ya usadizi wa jumuiya ya kimataifa lakini jukumu la kuhakikisha uchaguzi wa usalama linasalia la DRC na yafutayo ni muhimu

(SAUTI KOBLER)

‘‘Kwanza bajeti inahitajika  haraka, pili kalenda ya uchaguzi lazima iwe halisi na tatu uandikishaji wa wapiga  kura lazima uboreshwe kujumuisha mathalani vijana ambao wamefikia umri wa kupiga kura toka uchaguzi uliopita’’

Kuhusu nchi jirani ya Burundi Kobler amesema bado hali ni tete lakini akapongeza hatua za kutafuta suluhu nakutaka juhudi zaidi.