Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utolewaji wa elimu na upatikanaji wa maji umeongezeka duniani: Wu Hongbo

Utolewaji wa elimu na upatikanaji wa maji umeongezeka duniani: Wu Hongbo

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika idara ya  masuala ya kijamii na kiuchumi DESA, Wu Hongbo amesema tangu mwaka 1995 maisha ya raia kote duniani yameboreshwa kufuatia uetekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia MDGS.

Akiwasilisha ripoti ya utekelezaji wa MDGS mbele ya waandishi wa habari mjini New York Bwana Wu amesema mafaniko yako dhahiri katika elimu, kupunguza njaa, na kupunguza vifo vya watoto .

(SAUTI YA WU)

‘‘Njaa imepungua kwa takribani nusu ,wasichana wanahudhuria shuleni kuliko wakati wowote ule, vifo vya watoto walioko chini ya miaka mitano kimataifa imepungua kwa nusu.’’

Amesema maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi vimeoungua kwa asilimia 40 na hivyo kuepuka vifo vya mamilioni ya watu hatua ambayo ameeleza ni juhudi za mapambano dhidi ya ukimwi malaria na kifua kikuu.

Ameongeza kuwa katika upatikanaji wa maji tangu mwaka 1990 watu bilioni 2.6 wamepata maji safi ya kunywa huku wengine bilioni bilioni 1.2 wamepata huduma za kujisafi.