Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNRWA na EU wainua uchumi wa vijana wakimbizi Syria

UNRWA na EU wainua uchumi wa vijana wakimbizi Syria

Mpango wa mafunzo ya miradi ya vijana katika kituo cha mafunzo ya wakimbizi wa Kipalestina(UNRWA) mjini Damascus, Syria umeinua uchumi wa vijana wakimbizi, hatua iliyowawezesha kusaidia mahitaji ya familia zao. Taarifa kamili na Joseph Msami.

(TAARIFA YA MSAMI)

Mpango huo unaodhaminiwa na Umoja wa Ulaya(EU) unahusisha mafunzo ya majuma mawili kuhusu ajira katika matengenezo ya simu za mkononi na teknolojia yake kwa ujumla.

Mradi umewawezesha vijana waliokimbia nchi yao kutokana na machafuko, akiwamo Mohammad Alloh ambaye anasema kabla ya mafunzo hayo, alikuwa hawezi kulipa kodi ya nyumba ya mwezi mmoja kutokana na kipato kidogo kwa kazi ya msaidizi katika duka la simu za mikononi.

Mafunzo hayo ambayo pia yamehusisha ujuzi katika kuanzisha bishara, yamebadili maisha ya vijana kambini hapa, mathalani Mohammad ambaye baada ya kupata ujuzi huo pamoja na kasha maalum lenye vifaa vya matengenezo sasa anapokea kiasi cha Euro 95 hadi 142 kwa mwezi.

UNRWA pamoja na Umoja wa Ulaya EU katika mradi huu wanakusudia kuwawezesha vijana 33 ili kukabiliana na soko la ajira nchini Syria.