Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNIDO,CDB kukuza maendeleo ya viwanda Afrika

UNIDO,CDB kukuza maendeleo ya viwanda Afrika

Shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya viwanda UNIDO kwa kushirikiana na benki ya maendeleo ya China CDB zimeungana katika mkakati wa kukuza maendeleo jumuishi na endelevu ya viwanda katika nchi zinazoendelea zilizoko katika ukanda ambao ulikuwa ukifanya biashara na China kupitia bahari ya Hindi hadi Afrika.

Taarifa ya UNIDO inaeleza kuwa miongoni mwa nchi zilizojumuishwa katika ubia huo ni Ethiopia na Senegal ambazo ni sehemu ya  programu za UNIDO ambapo mkataba wa ubia huo umesainiwa hii leo mjini Addis Ababa ikiwa ni shemu ya juhudi za jukwaa la kuwekeza Afrika zinazofanywa na benki ya dunia na CDB pamoja na mfuko wa China- Afrika.

UNIDO na CDB zitafanya kazi kwa karibu katika maendeleo ya viwanda na kuimarisha mifumo na shughuli za kimaendeleo kwa ujumla pamoja na kuhuisha nishati kwa maendeleo imesema taarifa hiyo.

Akisisitiza hilo Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO Philippe Scholtes amesema mwanzo wa ushirikiano baina ya pande hizo unalenga katika ujenzi wa maendeleo endelevu na jumuishi katika kujengea uwezo nchi hususani barani Afrika ili kuendeleza miradi yakukuza uwekezaji kuanzia  nchi mbili za mfano ambazo ni Senegal na Ethiopia.