Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yajizatiti kukabiliana na njaa Sudan Kusini

WFP yajizatiti kukabiliana na njaa Sudan Kusini

Tangu kuanza kwa mzozo nchini Sudan Kusini Disemba 2013, takriban watu milioni mbili nchini humo wamesalia  wakimbizi wa ndani au wamekimbilia nchi jirani. Mazungumzo ya amani ya hivi majuzi hayajazaa matunda na mapigano yameongezeka huku ikiongeza idadi ya watu wanaohitaji msaada wa chakula. Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP linatumia mbinu mbali mbali kuwafikia wakimbizi hawa ikiwemo usafiri wa boti, mgao wa fedha na vocha kwa ajili ya watu wanaokabiliwa na njaa katika maeneo ya mzozo. Kadhalika WFP inawasilisha chakula kupita angani, kulikoni? Ungana na Grace Kaneiya katika makala hii