Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji 137,000 walivuka Bahari ya Mediterenia 2015

Wahamiaji 137,000 walivuka Bahari ya Mediterenia 2015

Idadi ya wahamiaji na wakimbizi waliovuka Bahari ya Mediterenia mwaka 2015 imevunja rekodi, ikiwa ni watu 137,000 waliongia Ulaya kati ya mwezi Januari na Juni, kulingana na ripoti iliyotolewa leo na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR. Taarifa kamili na Priscilla Lecomte

Taarifa ya Priscilla

Ripoti hiyo ya UNHCR imesema kuwa mizozo ndiyo sababu kubwa hasa ya idadi hiyo kubwa ya wakimbizi na wahamiaji waliofanya safari hatarishi za kuvuka Bahari ya Mediterenia, ingawa pia utesaji ulichangia.

Ripoti imesema pia kuwa idadi hiyo imezidi ile ya mwaka jana wakati kama huo kwa asilimia 80.

Nchi wanakotoka wengi wao ni Syria, Afghanistan na Eritrea.

Ripoti inasema idadi ya vifo baharini pia ilivunja rekodi mwezi Aprili, ambapo watu zaidi ya 1,300 walizama na kufa au kutoweka, ingawa idadi hiyo ilishuka mwezi Mei na Juni.