Skip to main content

Pengo la lishe bora kati ya nchi maskini na tajiri kupungua muongo ujao: Ripoti

Pengo la lishe bora kati ya nchi maskini na tajiri kupungua muongo ujao: Ripoti

Ripoti mpya iliyotolewa leo kuhusu sekta ya kilimo duniani imeonyesha matumaini ya kuimarika kwa lishe kwenye nchi zinazoendelea katika muongo mmoja ujao.

Ikipatiwa jina la mwelekeo wa kilimo kwa mwaka 2015 hadi 2024, ripoti hiyo ya shirika la chakula na kilimo duniani, FAO na lile la kiuchumi na maendeleo, OECD inasema kuna ongezeko la matumizi bora ya mlo sahihi katika nchi hizo na hivyo kupunguza pengo la lishe kati yao na nchi zilizoendelea.

Boubaker Ben-Belhassen, Mkurugenzi wa Kitengo cha biashara na masoko, FAO anasema hizo ni habari njema lakini…

(Sauti ya Boubaker)

Aina zingine za utapiamlo zinahitaji kutatuliwa kama utipwatipwa, uzito kupita kiasi na magonjwa yanayohusiana na lishe.”

Halikadhalika ripoti imeangazia mwelekeo wa bei ya mazao ikisema zitashuka na sababu ni pamoja na kuimarika kwa uzalishaji wa mazao, tija katika sekta ya kilimo na kudorora kwa ukuaji wa uchumi duniani.

Hata hivyo ripoti inasema licha ya matumaini  hayo ni lazima kuendelea kuwa macho kwa kuwa chochote kinaweza kutokea na kusababisha bei za mazao kupanda.