Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lalaani mauaji ya mwendesha mashtaka Misri

Baraza la usalama lalaani mauaji ya mwendesha mashtaka Misri

Baraza la usalama limeaalani vikali mauaji ya mwendesha mashtaka wa umma wa Misri Hisham Barakat yaliyotokana na shambulio la kigaidi la bomu lililenga msafara wake na kujeruhi vibaya watu wengine.

Taaarifa ya wajumbe wa baraza la usalama imesema wametuma salamu za rambirambi kwa familia ya waathiriwa na kwa watu wa serikali ya Misri na kusisistiza umuhimu wa kuwachukulia hatua za kisheria watekelezaji wa shambuio hilo.

Wamesisitiza pia umuhimu wa kupambana na aina zote za vitisho vya amani na usalama wa kimataifa  ambavyo vinasababishwa na vitendo vya ugaidi kwa mujibu wa katiba ya Umoja wa Mataifa na kuwa vitendo vyovyote vya jinsi hiyo bila kujali nia, vinapotekelezwa na hutekelezwa na  nani havikubaliki.

Wajumbe wa baraza la usalama wamekumbusha nchi kuwa lazima zihakikishe hatua za kukabiliana ugaidi lazima zizingatie sheria za kimataifa na haki za binadamu,za wakimbizi na sheria za kibinadamu.