Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama laongeza vikwazo Eritrea

Baraza la Usalama laongeza vikwazo Eritrea

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeongezea vikwazo taifa la Eritrea kwa kuunga mkono makundi ya wanamgambo yanayoendesha mapigano nchini Somalia na kuzua msukosuko kwenye sehemu kadhaa za pembe ya Afrika. Vikwazo hivyo vipya viko kwenye azimio lililoungwa mkono na wanachama 13 kati ya wanachama 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Azimio hilo limeitaka serikali ya Eritrea kukoma kutumia ushuru kutoka kwa raia wa Eritrea wanaoishi ng'ambo katika kununua silaha na kuitaka kuweka wazi fedha zinazotokana na sekta ya madini. Susan Rice ni balozi wa Marekani kwenye UM.

(SAUTI YA SUSAN RICE)