Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNMISS yagundua ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu Sudani Kusini

UNMISS yagundua ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu Sudani Kusini

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini umebaini ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu uliosambaa nchini humo na kudaiwa kufanywa na kikosi cha jeshi la SPLA na vikosi vyake katika mapugano ya hivi kativui jimnoni Unity. Tarifa zaidi na Joseph Msami.

(TAARIFA YA MSAMI)

UNMISS imewahoji waathiriwa 115 na mashuhuda wengine kutoka maeneo mbalimabli ya jimboni Unity ambapo SPLA ilianzisha mashambulizi makubwa dhidi ya vikosi vya upinzani mwishoni mwa mwezi Aprili na kubaini pamoja na mambo mengine wanawake 172 walitekwa huku wengine 79 walifanyiwa ukatili wa kingono ikiwamo kubakwa.

Katika mahojiano na Gabriel Shadar wa redio Miaraya ya UNMISS Kaimu msemaji wa UNMISS Joe Contreras anaeleza hatua inayofuata.

(SAUTI JOE)

‘‘Kwanza kabisa tunatumaini tunatumaini tutaruhusiwa vyema kupenya katika maeneo ya machafuko katika majuma yajayo. Tunatoa wito kwa kwa pande husika kuwachukulia hatua waliokiuka haki hizi za binadamu na kuchunguza kwa kina matukio haya. Ukiukwaji huu ni wa kusikitisha sana.’’

Takribani raia 67 waliuwawa kwenye mapigano hayo, wengine kuporwa huku zaidi ya watu 100,000 wakipoteza makazi.