Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya tabianchi kubadili virutubisho kwenye mazao: FAO

Mabadiliko ya tabianchi kubadili virutubisho kwenye mazao: FAO

Chapisho jipya la shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limesema ongezeko la joto duniani litaathiri jinsi chakula kinavyozalishwa halikadhalika kinapozalishwa na kusababisha kupungua kwa virutubisho kwenye vyakula.

Chapisho linafuatia tafiti za madhara ya mabadiliko  ya tabianchi kwenye sekta ya chakula na kilimo katika miongo miwili iliyopita, likieleza kuwa hali ya joto na ukame kwenye maeneo karibu na Ikweta yanaweza kupunguza uzalishaji wa chakula huku joto kiasi kwingineko likanufaisha uzalishaji kwa kiasi, waathirika zaidi zikiwa ni nchi za vipato vya chini.

Aziz Elbehri, mhariri wa chapisho hilo na pia afisa kutoka kitengo cha biashara na masoko cha FAO anaenda mbali zaidi kubainisha jinsi ongezeko la joto linavyopunguza virutubisho muhimu kwenye mchele na ngano..

(Sauti ya Aziz)

Mazao haya yanabainika kukosa Zinki na protini na badala yake kujaa zaidi wanga. Sasa ukichukulia India, vyakula hivyo ni mlo mkuu kwa theluthi moja ya wakazi wa vijijini kwa hiyo wanakuwa hatarini kukumbwa na utapiamlo na ukosefu wa Protini.”