Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muda changamoto kuelekea mkataba mpya wa mabadiliko ya tabia nchi

Muda changamoto kuelekea mkataba mpya wa mabadiliko ya tabia nchi

Muda hautoshi kuelekea katika makubaliano mapya ya kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi ambayo yanatarajiwa kupitishwa mwezi Disemba amesema msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu mabadiliko ya tabia nchi Janos Pasztor katika mkutano na wandishi wa habari mjini New York

Bwan Pasztor alikuwa akizungumzia juhudi za jumuiya ya kimataifa katika kupigia chepuo harakati dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi ikiwa ni siku zisizozidi 200 kabla ya kongamano la Umoja wa Mataifa kuhusu mada hiyo mjini  Paris nchini Ufaransa mwezi Desemba.

Kiongozi huyo wa mabadiliko ya tabia nchi akasisistiza kile kilichofikiwa katika mikutano baina ya nchi ikiw ani sehmu ya maandalizi.

(SAUTI PASZTOR)

"Hatua dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi zaweza kuzuia mabadiliko hayo lakini tukisubiri itakuwa ngumu na garama zaidi. Ni dhahiri kuwa Katibu Mkuu anapigia chepuo juhudi za kimataifa ambazo sio tu zitashughulikia mabadiliko ya tabia nchi lakini pia kukuza ukuaji wa uchumi, fursa ya kiafya, elimu na ajira."

 Ameonya kuwa ikiwa hatua hazitachukuliwa joto kimataifa litaongezeka zaidi ya kiwango cha nyuzi joto mbili kwa kipimo cha Celsius kilichowekwa na jumuiya ya kimataifa.