Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dunia nzima ishiriki harakati za kutokomeza njaa:FAO

Dunia nzima ishiriki harakati za kutokomeza njaa:FAO

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la chakula na kilimo duniani, FAO Jose Graziano da Silva ametoa shime kwa ulimwengu mzima kushiriki katika kutokomeza njaa na utapiamlo.Joshua Mmali na maelezo zaidi.

(Taarifa ya Joshua)

Amesema hayo wakati akifungua jukwaa la kimataifa la kilimo katika maonyesho ya Milan, EXPO Milano 2015 linalofanyika wakati huu ambao ni  hitimisho la miaka 15 ya kumaliza njaa na duniani na kuanza kwa lengo jipya endelevu la kutokomeza kabisa njaa na kufikia uhakika wa chakula na lishe.

Kwa mantiki hiyo Da Silva amesema mafanikio yamepatikana kwa lengo la milenia lakini anarejelea wito kwa washiriki kufikia lengo jipya safari inapoanza ya kutekeleza.

Bwana Da Silva amesema msingi wa njaa siyo uhaba wa chakula bali umaskini ambao unachochewa na ukosefu wa usawa na unajikita katika masuala ya ukosefu wa maji, ardhi, masoko na zana nyingine za uzalishaji

Amesema Umoja wa Mataifa kwa upande wake unatoa msaada wa dhati kwa zaidi ya nchi 100 Afrika, Amerika ya Kusini na Asia ambazo tayari zimejizatiti kutokomeza njaa.