Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanamuziki wanufaikeje vya kutosha na matunda ya jasho lao?

Wanamuziki wanufaikeje vya kutosha na matunda ya jasho lao?

Muziki kama zilivyo kazi nyingine za sanaa, huelimisha, huburudisha na hata kuhabarisha. Watunzi hukeshwa kutwa kucha wakipanga mashairi bora na mbinu bora za kufikisha ujumbe huo. Hata hivyo mara nyingi hasa katika nchi zinazoendelea, matunda ya kazi yao huwa nadra sana kupata na hata wakipata yanakuwa kidogo kulinganisha na jasho ambalo limewatoka. Sasa sauti zinapaswa kila wakati ili nao wale matunda ya jasho lao kama inavyobainisha makala hii iliyoandaliwa na Amina Hassan akimuangazia mwanamuziki nguli Ismaël Lô.