Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mitaala kuhusu matumizi ya mitandao ijumuishwe kwenye masomo: WSIS

Mitaala kuhusu matumizi ya mitandao ijumuishwe kwenye masomo: WSIS

Wakati jukwaa la dunia kuhusu jamii na mawasiliano ulimwenguni, WSIS, likiendelea huko Geneva, Uswisi imebainika kuwa idadi kubwa ya watumiaji wa mtandao wa intaneti ikiwemo mitandao ya kijamii, mathalani barani Afrika, hawana ufahamu na uelewa wa kutosha kuhusu matumizi yake na hivyo kuhatarisha usalama sio wao tu bali wa mali zao na jamaa zao.

Hiyo ni kwa mujibu wa Meneja mawasiliano wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA Innocent Mungy ambaye anashiriki mkutano huo akiwakilisha Tanzania ambapo amesema ukosefu wa uelewa wa kutosha husababisha watu kuchapisha taarifa ambazo huangukia mikononi mwa wahalifu wa mitandaoni.

(Sauti ya Bwana Mungy)

Ili kuondokana na hali hiyo jukwaa limetoa mapendekezo.

(Sauti ya Bwana Mungy)

Jukwaa hilo, WSIS limeandaliwa kwa pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la mawasiliano, ITU, elimu na utamaduni, UNESCO, kamati ya biashara na maendeleo UNCTAD na mpango wa maendeleo, UNDP.

Maudhui ya jukwaa hilo ni ubunifu pamoja, wezesha Tehama kwa maendeleo endelevu.