Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki za wasanii wa muziki zizingatiwe ili tuendelee kufurahia muziki: WIPO

Haki za wasanii wa muziki zizingatiwe ili tuendelee kufurahia muziki: WIPO

Huu ni muziki ulioporomoshwa a wasaani wa Afrika Kusini katika maadhimisho ya siku ya hakimiliki duniani, ambayo siku yenyewe ni Aprili, 26 na maudhui ya mwaka huu ni mustakhabali wa muziki katika nyakati za sasa.

Katika ujumbe alioutoa kwa mwaka huu, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hakimiliki duniani WIPO, Francis Gurry amesema teknolojia za digitali na mtandao wa intaneti vimewezesha watu wote duniani kusikiliza muziki wowote kwa wakati wowote.

Lakini ameeleza kwamba mabadiliko hayo yameathiri pia wasanii wenyewe ambao hawapati tena riziki ya kutosha kutokana na usaani wao.

Bwana Gurry amezingatia kwamba ni lazima kila mtu athamini muziki ili kuweza kuendelea kufurahia kuusikiliza, na kwa hiyo ni lazima jamii ya kimataifa ibuni jinsi ya kuwapatia wasanii malipo ya kutosha ili biashara ya muziki iwe endelevu.