Skip to main content

Uchochezi hauwezi kutatuliwa na viongozi wa dini pekee

Uchochezi hauwezi kutatuliwa na viongozi wa dini pekee

Mkutano kuhusu nafasi ya viongozi wa dini katika kuzuia uchochezi unaoweza kusababisha vitendo vya ukatili umemalizika leo mjini Fez nchini Morocco kwa wito kwa viongozi wa taasisi za kidini kushirikiana na tasisi nyingine za kijamii katika kukomesha chuki . Taarifa zaidi na Assumpta Massoi

(TAARIFA YA ASSUMPTA)

Miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo wa siku mbili ni pamoja na Mohamed Abu-Elnimr ambaye ni mshauri maalum wa taasisi ya mfalme Abdulla wa pili KAACID na pia Profesa katika chuo kikuu cha Amerika huko Washington.

Profesa Mohamed ameiambia redio ya Umoja wa Mataifa baada ya kumalizika kwa mkutano huo kuwa,  uchochezi unaosababisha ghasia ni suala mtambuka

(SAUTI Profesa MOHAMED)

"Viongozi wa dini sio sababu pekee ya kauli chochezi , utafiti unaonyesha kuwa kwa asilimia kubwa ni wanasiasa na watu katika sehemu zenye migogoro wakitumia dini katika muktadha huo.

Amesema katika kutafuta ufumbuzi wa uchochezi kama huo lazima taasisi nyingi kama vile za kisiasa na kijeshi zihusishwe kikamilifu.