Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Madhara ya mabadiliko ya tabia nchi yapaswa kushughulikiwa: FAO

Madhara ya mabadiliko ya tabia nchi yapaswa kushughulikiwa: FAO

Juhudi za pamoja zinahitajika ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo yana madhara ya moja kwa moja kwa maisha ya watu amesema mkuu wa shirika la chakula na kilimo FAO Jose Graziano da Silva.

Katika taarifa yake Bwana da Silva amesema pale ambapo kilimo hakina fursa ya kustawi na kukiwa na ukosefu wa chakula madhara yako dhahiri.

Amesema njaa yaweza kusababisha watu kuacha familia zao na nyumba zao katika jitihada za kusaka fursa bora ambazo hata hivyo hawazipati mara zote. Ametolea mfano wa vifo vya wahamiaji na wasaka hifadhi katika bahari ya Mediterranean. Pia ametolea mfano wa kimbunga Vanuatu na kile cha nchini Ufilipino akionyesha jinsi ambavyo mazao ya chakula yaweza kuharibiwa haraka kutokana na matukio ya hali mbaya ya hewa.

Mkuu huyo wa FAO alikuwa akizungumza katika bunge la Italia ambapo amewaeleza wajumbe wa bunge akiwamo waziri wa mazingira kuwa FAO inasikitishwa na kufuatilia mabadiliko ya tabianachi kutokana na mahusiano yake ya moja kwa moja na usalama wa chakula na kilimo.