Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano kuhusu usalama wa boti zinazosafirisha watu kufanyika Ufilipino:IMO

Mkutano kuhusu usalama wa boti zinazosafirisha watu kufanyika Ufilipino:IMO

Shirika la kimataifa la masauala ya majini IMO, limesema litafanya mkutano kuhusu uboreshaji wa usalama wa meli na boti zinazosafirisha abiria katika safari za ndani . Mkutano huo utafanyika mjini Manila Ufilipino April. 24 mwaka huu.Mkutano huo ambao utafunguliwa na Katibu Mkuu wa IMO The Koji Sekimizu,mwenyeji wake ni serikali ya Ufilipino, na unatarajiwa kuhudhuriwa na nchi wanachama wa IMO wanaouguswa na suala hilo, pia wawakilishi  wa mashirika ya kikanda na mashirika ya kimataifa yasiyo ya kiserikali yaani NGO’s.

Mkutano unatarajiwa kufikiria mswada wa  muongozo kuhusu operesheni salama za kusafirisha abiria katika maeneo ya pwani na miongoni mwa visiwa , safari zisizo za kimataifa.

Muongozo huo utajikita katika ununuzi wa boti chakavu, mabadiliko ya idadi ya safari, ukarabati wa boti kabla hazijaanza safari, uhesabu wa abiria na mpango wa safari.