Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maendeleo endelevu ni kitovu cha uchumi wa dunia: Wu Hongbo

Maendeleo endelevu ni kitovu cha uchumi wa dunia: Wu Hongbo

Mkutano kuhusu biashara na maendeleo ulioandaliwa na baraza la uchumi na kijamii, benki ya dunia, shirika la kimtaifa la biashara WTO pamoja na mfuko wa kimataifa wa fedha umefanyika leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni mkuu wa idara ya Umoja wa Mataifa ya uchumi na maswala ya kijamii DESA Wu Hongbo ameuambia mkutano huo kuwa ajenda ya maendeleo endelevu inayosukuma ulimwengu kwa sasa inalenga kuleta mabadiliko duniani katika maeneo nyeti kama vile.

(SAUTI)

"Kupunguza njaa na umaskini, elimu biora, afya, usawa wa kijinsia na upatikanaji wa maji, nishati na huduam za kujisafi, ajira na  miundombinu na ukosefu wa usawa."

Amesisitiza kuwa mjadala katika mkutano huo ujikite zaidi katika uwezeshaji wa maendeleo endelevu ili kuleta mabadiliko ya kiuchumi duniani.