Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bado hali tete Yarmouk, tunahaha kunusuru: UNRWA

Bado hali tete Yarmouk, tunahaha kunusuru: UNRWA

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa  Kipalestina UNRWA, limesema linahaha kutoa misaada kunusuru maisha ya wakimbizi waliozingirwa  katika kambi ya Yarmouk nchini Syria

Kwa mujibu wa msemaji wa UNRWA mjini Yerusalem Chris Gunness,  wanaume, wanawake na watoto wa Palestian na Syria waliozingirwa kambini humo bado hawapati mahitaji muhimu kama vile chakula, maji, na huduma za afaya kutokana na machafuko yanayoendelea na akataka wanadiplomasia , wachumi na hata viongozi wa kidini kuwashawishi vikundi kinzani kusitisha mapigano.

(SAUTI YA GUNNESS)

"Tuna  taarifa ambazo hazijathibitishwa kuhusu ulipuliwaji wa mabomu kutoka angani, ndiyo maana tunasema dunia haiwezi kukaa kimya na isifanye lolote."

Bwana Gunness,  amesema hata hivyo hawajakata tamaa ya usaidizi na kwa sasa wamejikita katika eneo liitwalo Tadamon na kutoa makasha yenye vifaa vya huduma za kujisafi kwa watu wazima na watoto, na huduma za afya kwa ajili ya familia zilizosalia baada ya  kutoweka kutoka Yarmouk mnamo April nne mwaka huu