Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shehena ya kwanza ya vifaa tiba yawasili Yemen: UNICEF

Shehena ya kwanza ya vifaa tiba yawasili Yemen: UNICEF

Wakati hali ya kibinadamu inazidi kuzorota nchini Yemen kila uchao, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF limefanikiwa kufikisha vifaa tiba na vingine ili kusaidia maelfu ya watoto na familia zao. Taarifa kamili na John Kibego

 (Taarifa ya John Kibego)

Ndege iliyoondoka kwenye kituo cha vifaa cha UNICEF nchini Denmark na tani 16 za vifaa tiba imewasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sana’a nchini Yemen hii leo.

Shehena hiyo ni pamoja na dawa, mabomba ya sindano na bandeji inalenga kusaidia  takriban watu 80,000 pamoja na virutubisho kwa ajili ya watoto 20,000 na vyombo vya kuhifadhia maji.

Christopher Boulierac ni msemaji wa UNICEF Geneva.

(Sauti ya Boulierac)

“Tani 16, hasa vifaa vya matibabu, na vifaa vya kusafisha maji, kujisafi, na  kushughulikia maji machafu. Yaani sina maelezo zaidi kuhusu usambazaji lakini mpango ni kuwa vifaa hivyo visambazwe sasa hivi, haraka iwezekanavyo, kwenye maeneo yaliyoathirika na mapigano, kwa ajili ya walengwa”