Skip to main content

Rasilimali fedha na watu vyakwamisha misaada Sudan Kusini

Rasilimali fedha na watu vyakwamisha misaada Sudan Kusini

Ukosefu wa fedha na wafanyakazi waliofunzwa unakwamisha juhudi za usaidizi wa janga la kibinadamu Sudan Kusini amesema afisa wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA Vincent Lelei nchini Sudan Kusini.

Bwana Lelei amesema OCHA inahitaji kugawa misaada kwa wakimbizi wa ndani mathalani madawa, mbegu za kupandia mazao, maji safi na chakula.

(SAUTI LELEI)

"Tunahitaji uwezeshaji mkubwa zaidi kwakuwa kiwango cha uhitaji ni kikubwa zaidi na tunahitaji watu wenye ujuzi zaidi katika kila sekta ambapo usaidizi unahitajika."

Mamia kwa maelfu ya watu wamepoteza makazi kufuatia mapigano kati ya vikosi vya serikali na wapinzani yalioanza mwaka 2013.