Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kumbukizi ya mauaji ya kimbari Rwanda itupe funzo: Ban

Kumbukizi ya mauaji ya kimbari Rwanda itupe funzo: Ban

Katika kumbukizi ya mauaji ya Rwanda iliyofanyika jumanne, tarehe 7, Aprili, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekariri mshikamano wa Umoja wa Mataifa na raia wa Rwanda, akisisitiza umuhimu wa kujifunza kutokana na mateso hayo na kuwajibika:

“Haitoshi kulaani mauaji yanapotokea. Tunapaswa kuchukua hatua mapema zaidi kuyazuia”

Kwa upande wake mwakilishi wa kudumu wa Marekani kwenye Umoja, Balozi Samantha Power amesema somo la msingi ni kwamba mauaji ya kimbari yaliyofanyika Rwanda yangeweza kuzuiliwa, iwapo jamii ya kimataifa ingechukua hatua mapema. Akihadithia jinsi wanafunzi wa Rwanda walivyouwawa kwa msingi wa kabila lao la kitutsi, kwenye chuo kikuu cha Butare, akasema:

“ Tukitafakari yaliyotokea, tunapaswa kuzuia mauaji yasitokee wakati wa sasa. Hata hivyo, tukisikiliza kwamba wanafunzi wa chuo kikuu wa Kenya, Garissa, ambao wamevutwa nje ya mabweni yao na kuawa, je hatushtuki kama tunavyoshtuka tukihaditihia tena mauaji ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Butare?”