Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa OCHA – DRC alaani mashambulizi dhidi ya wakimbizi wa ndani

Mkuu wa OCHA – DRC alaani mashambulizi dhidi ya wakimbizi wa ndani

Kaimu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu Misaada ya Kibinadamu, OCHA nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Joseph Inganji, amelaani mashambulizi manne yaliyotokea katika kipindi cha mwezi Machi pekee Mashariki mwa DRC.

Bwana Inganji amesema waasi wamekiuka haki za binadamu na sheria ya kibinadamu katika mashambulizi hayo yaliyofanyika dhidi ya kambi za wakimbizi wa ndani, ambapo watu wamejeruhiwa, wanawake kubakwa na mali kuharibiwa na kuibiwa.

Mratibu huyu wa Umoja wa Mataifa amezingatia kwamba kambi hizo na wakimbizi wenyewe wanapaswa kulindwa kwa mujibu wa sheria ya kimataifa ya kibinadamu

Bwana Inganji amezisihi mamlaka za serikali ya DRC kuhakikisha kwamba wakimbizi wa ndani wanalindwa na watekelezaji wa uhalifu huu wanapelekwa mbele ya sheria.