Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yazindua chombo cha kurahisisha upatikanaji wa takwimu zake

UNICEF yazindua chombo cha kurahisisha upatikanaji wa takwimu zake

Shirika la Kuhudumia Watoto katika Umoja wa Mataifa, UNICEF limebadilisha tovuti zake za takwimu ili kuwezesha upatikanaji rahisi wa takwimu zake kuhusu afya, lishe, elimu, maji na huduma za kujisafi, ulinzi wa watoto na HIV na Ukimwi.

Takwimu hizo sasa zimewekwa katika muundo ambao unajumuisha maelezo kuhusu nchi na chombo cha kuonyesha picha za takwimu zikiwekwa katika ramani na grafu

Taarifa ya UNICEF imesema muundo huu mpya utaifanya UNICEF kuwa chanzo cha kutegemewa kwa takwimu zote kuhusu wanawake na watoto.

UNICEF imesema, matatizo ambayo hutokea bila kupimwa, aghalabu hupita bila kutatuliwa, ikiongeza kuwa takwimu za mara kwa mara na za kutegemewa kuhusu watoto, familia zao na jamii zao ni muhimu katika kuboresha maisha yao na nguzo ya kutimiza haki zao.